Mshumaa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mshumaa ukinunuliwa dukani huko Zambia.
Mvulana na mshumaa, mchoro wa Michel Gobin.
Mkusanyo wa mishumaa ya kikemikali ya kisasa.

Mshumaa (kwa Kiingereza candle, kutokana na Kilatini candēla, neno ambalo linategemea kitenzi candēre, kuangaza.[1]) ni kifaa cha kuletea mwanga gizani kinachotengenezwa kwa nta au kemikali fulani.

Unaweza kuwashwa pia kwa sababu ya kuleta harufu au joto, au hata kwa kupima muda[2].

Ili kushika mshumaa, tangu zamani vilitengenezwa vinara vya thamani tofautitofauti na hata vilivyopambwa kwa sanaa.[3]

Mshumaa unawashwa kwa kiberiti, halafu unaendelea wenyewe huku ukiyeyuka taratibu.[4]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mishumaa ya zamani zaidi kati ya ile iliyopo hadi leo ilitengenezwa huko China miaka 200 KK hivi, na ilifanywa kwa mafuta ya nyangumi.[5]

Mshumaa ukiwaka katika monasteri ya Visoki Dečani.

Kabla ya kuvumbua namna ya kutengeneza umeme, mishumaa na taa za mafuta ndivyo vilivyotumika kuleta mwanga, kama ilivyo bado umeme huo usipopatikana.

Lakini katika nchi zilizoendelea, mishumaa inatumika bado kwa mapambo tu, hasa mahali pa ibada au kuhusiana nayo. [6] Muhimu kuliko yote ni mshumaa wa Pasaka.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Candle". The Free Dictionary By Farlex. Iliwekwa mnamo 2012-05-19. 
  2. Whitrow, G. J. (1989). Time in History: Views of Time from Prehistory to the Present Day. Oxford University Press. ku. 90–91. ISBN 0-19-285211-6. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-06-10. Iliwekwa mnamo 2015-12-23. 
  3. "chandelier". The Free Dictionary By Farlex. Iliwekwa mnamo 2012-05-19. 
  4. European Candle Association FAQ Archived 13 Januari 2012 at the Wayback Machine..
  5. Forbes, R J (1955). Studies in Ancient technology. ku. 139–140. ISBN 9789004006263. Iliwekwa mnamo 7 November 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  6. Geddes, Gordon; Jane Griffiths. Christianity. Heinemann. uk. 89. ISBN 0-435-30693-6. 

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Franz Willhöft, Rudolf Horn, Ullmann's Encyclopedia of Industrial Chemistry, "Candles", ed. Wiley-VCH, ed. 6, 2003, ISBN= 3-527-30385-5

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.